DW imechagua Kiswahili kama lugha ya mawasiliano
Wrong language? Change it here.

Matukio ya Kisiasa

Vuguvugu Nigeria lataka jimbo la Biafra lijitenge

ImageBaada ya kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la Biafra nchini Nigeria yaliyosababisha vifo vya watu milioni moja, vuguvugu kusini mashariki mwa nchi hiyo linataka jimbo la Biafra lijitawale.

Matukio ya Kisiasa

Obama: Nitahakikisha mkataba imara unapatikana

Rais Barack Obama wa Marekani amesema dunia inahitaji mfumo wa kudumu kwa ajili ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi na atahakikisha unapatikana mkataba utakaoimarisha uchumi na kusaidia kulinda mazingira ya dunia.

Matukio ya Kisiasa

Jitihada za kupunguza ongezeko la joto zaendelea

Siku moja baada ya viongozi wa dunia kuonyesha dhamira ya kuungana katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wanaendelea na mazungumzo muhimu.

Matukio ya Kisiasa

Urusi yasema haitaki vita na Uturuki

Waziri wa Uturuki anayeshughulikia uhusiano na Umoja wa Ulaya amesema nchi yake haiwezi kuwa na uhusiano wa kiadui na Urusi, baada ya ndege ya kijeshi ya Urusi kutunguliwa na Uturuki.

Matukio ya Kisiasa

Papa: Wakristo na Waislamu ni ndugu

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis amesema Wakristo na Waislamu ni ndugu, hivyo amewataka wakatae chuki na kuungana pamoja kupinga ghasia zinazofanywa kwa kisingizio cha kutumia jina la dini.

Matukio ya Afrika

Maoni : Mwanzo mpya Burkina Faso na mtu anayefahamika

Rais mpya wa Burkina Faso ana kazi kubwa ya ujenzi mpya. Muhimu zaidi katika kazi hiyo ni kurekebisha uhalifu uliotokea wakati wa kipindi cha utawala wa mtangulizi wake.

Matukio ya Afrika

Mahakama ya ICTR yafungwa Arusha

Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyoko Arusha ilikuwa ikishughulikia kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita na kuwasikiliza watuhumiwa wa mauaji ya kimbari.

Matukio ya Afrika

Rushwa imeongezeka Afrika

Rushwa inaathiri maendeleo katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara , ambako watu wanaokadiriwa kufikia milioni 75 wametoa rushwa katika mwaka mmoja uliopita.

Matukio ya Afrika

Mmoja afa baada ya zoezi la kiusalama Kenya

Polisi nchini Kenya inachunguza zoezi la kupima utayari wa kukabiliana na shambulizi la magaidi katika chuo kikuu cha Strathmore Nairobi, ambapo mtu mmoja alifariki na zaidi ya wanafunzi 20 kujeruhiwa.

Matukio ya Afrika

Kabore ni rais mteule wa Burkina Faso

Waziri mkuu wa zamani wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kabore, ameshinda uchaguzi wa Rais uliofanyika mwaka mmoja baada ya Blaise Compaore kutolewa madarakani kufuatia maandamano ya kumpinga.

Masuala ya Jamii

"Serikali isaidie vituo vya yatima wa Ukimwi"

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Ukimwi, DW imezungumza na Hellen Nkunda anayeendesha kituo cha yatima Tanzania. Anasema serikali lazima itoe msaada zaidi kwa watoto waliopoteza wazazi kwa Ukimwi.

Masuala ya Jamii

Magufuli na Papa Francis wavuma Twitter

Watumiaji wa Twitter Afrika Mashariki wameijadili ziara ya Papa na kuonyesha Magufuli anavyowafanya wabane matumizi. Katika Sema Uvume tunazungumzia mada hizo na kukufahamisha kuhusu App ya DW.

Masuala ya Jamii

Fahamu zaidi kuhusu mtoto wa jicho

Je, nini tatizo la mtoto wa jicho na je, athari zake kwa mgonjwa ni zipi?

Masuala ya Jamii

Papa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Papa Francis ametoa mwito wa amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Jumapili (29.11.2015) alipotembelea kambi za watu walioachwa bila makaazi

Masuala ya Jamii

Papa awasili Jamhuri ya Afrika ya Kati akitokea Uganda

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amekamilisha ziara yake nchini Uganda na asubuhi ya leo (29.11.2015) alielekea Jamhuri ya afrika ya kati alikowasili muda mfupi uliopita.

Michezo

Wenger hasikitiki kuhatarisha kuumia Sanchez

Kocha wa Arsenal Aserne Wenger amesisitiza kwamba hasikitiki kwa kuhatarisha kuumia kwa Alexis Sanchez katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Norwich City

Michezo

Gianni Infantino alenga kuisafisha FIFA

Giani Infantino mgombea wa kiti cha urais kutoka shirikisho la kandanda la mataifa ya Ulaya UEFA amesema atafanya kazi kuisafisha FIFA kuanzia siku ya kwanza, iwapo atachaguliwa

Michezo

Klitschko ataka pigano la marudiano na Fury

Aliyekuwa bingwa wa dunia wa uzani mzito Wladimir Klitschko ameomba waandalizi wa ndondi kumpa nafasi ya kuzichapa tena dhidi ya muingereza Tyson Fury hapo mwakani.

Michezo

Murray aisaidia Uingereza kushinda Davis Cup

Andy Murray ameisaidia timu ya taifa ya tennis ya Uingereza kunyakua kwa mara ya kwanza katika historia kombe la Davis la mchezo wa tennis mwishoni mwa juma baada ya kusubiri kwa muda wa miaka 77.

Michezo

Hamburg yapinga kuandaa michezo ya Olimpiki

Wakaazi wa mji wa Hamburg wamekataa michezo ya olimpiki ya majira ya joto ya mwaka 2024 isifanyike katika mji wao baada ya kupiga kura ya maoni

Michezo

Bayern yaendelea kuvunja rekodi

Bayern Munich imeendelea kuvunja rekodi katika Bundesliga kwa ushindi wa 13 katika michezo 14 ya ligi hiyo baada ya kuishinda Bertha Berlin kwa mabao 2-0. Hivyo wanaongoza kilele ni pointi 40