1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

[No title]

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcD

Kuna taarifa kuwa ndege za kijeshi za Marekani zinazoongozwa kwa mitambo maalum, zimeshambulia maeneo ya kusini mwa Somalia kunakohisiwa kujificha wapiganaji wa kundi la Al Qaida.

Taarifa zilizotolewa na kituo cha television cha Marekani cha CBS zimesema kuwa ndege hizo kutoka katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko Djibout zimeshambulia maeneo hayo kuwasaka wapiganaji wa Al Qaida waliyokuwa wakiwasaidia wapiganaji wa muungano wa mahakama za kiislam.

Hata hivyo hakuna taarifa zozote iwapo mashambulizi hayo yalifanikiwa malengo yake.

Lakini taarifa nyingine zinasema kuwa miili mingi ya watu ilionekana imetapakaa baada ya shambulizi hilo

Ndege hizo za Marekani zina bunduki zinazojifyatua zenyewe zikiwa na uwezo wa kutoa risasi elfu moja kwa sekunde.

Mpaka sasa Wizara wa Ulinzi ya Marekani haijasema lolote juu ya shambulizi hilo.

Wapiganaji hao wa Al Qaida ambao hawakutajwa majina ni pamoja na watuhumiwa wa ulipuaji wa balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.

Wakati huo huo Rais Abdullahi Yusouf wa Serikali ya Mpito ya Somalia jana aliwasili mjini Mogadishu ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 2004 alipochaguliwa.