1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

[No title]

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdN

Kikosi cha jeshi la majini cha Marekani kinawasaka wapiganaji wa mahakama za kiislam nchini Somalia wanaohisiwa kuwa na uhusiano na kikundi cha Al-Qaider.

Idara ya usalama ya Marekani imesema kuwa wana wasi wasi kuwa watuhumiwa wenye mahusiano na mitandao ya kigaidi ukiwemo wa Al-Qaider, ambao walihusika na ulipuaji wa balozi za marekani huko Tanzania na Kenya mwaka 1998 wanajaribu kukimbia Somalia.

Helicopta za jeshi la Marekani lililoko Djibout zimekuwa zikivinjari katika pwani ya pembe ya afrika kuwasaka wapiganaji hao.

Kenya imefunga mpaka wake na Somalia kuzuia kile ilichokisema uingizwaji wa silaha na wapiganaji wa kiislam wanaokimbia nchi hiyo baada ya majeshi ya serikali ya mpito yakisaidiwa na Ethiopea kutwaa miji yote ya Somalia.

Hata hivyo shirika la wakimbizi la umaja wa mataifa UNHCR limeilaumu serikali ya Kenya kwa hatua hiyo.

Lakini kwa upande wake mbunge wa jimbo la Dijis nchini Kenya mpakani na Somalia ambaye ni msomali Hussein Maalim ameunga mkono hatua hiyo, na amewataka wasomali kutanzua mzozo huo.

Wakati huo huo,umoja wa ulaya umetoa wito kwa serikali ya mpito na wapiganaji wa kiislam kurejea katika mazungumzo ya kutafuta amani nchini Somalia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ambayo ndiyo mwenyekiti wa umoja wa ulaya, Frank-Walter Steinmeir, amesema hatua za kijeshi zilizochukuliwa kwa kuungwa mkono na Ethiopea zinatoa nafasi kwa hatua za kidiplomasia kuchukuliwa katika kutanzua mzozo huo.

Na hayo yakiendelea taarifa kutoka Somalia zasema kwamba watu wenye silaha wamelishambulia kwa maguruneti lori la mafuta na kulilipua, ambapo watu watatu wamejeruhiwa