1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

[No title]

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIls

RIYADH:

Watu 10 wameuwawa pale moto uliporipuka katika bomba la gesi karibu na kinu cha gesi cha Hawiyah, nchini saudi Arabia jana usiku.

ARAMCO-kiwanda cha serikali cha mafuta na gesi kimesema katika taarifa yake kuwa moto huo ulisababishwa na kuvuja kwa gesi katika bomba liliopo km 30 kutoka kiwanda hicho.Moto huo sasa umedhibitiwa.