Wanajeshi wa Syria wampiga risasi na kumuua mtu mmoja ndani ya Lebanon katika bonde la Mashariki la Bakaa katika kampeni yao ya kuzima maandamano.
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baadhi ya wakaazi wa mashariki mwa nchi hiyo wanaelezea hofu yao muda mfupi baada ya kuondoka kwa askari wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO/ Wiki ya kupambana na ugonjwa wa Malaria
Tanzania yafanya majaribio ya kwanza ya treni ya mwendo kasi inayotumia umeme kati ya jiji la Dar es Salaam na Mji Mkuu Dodoma. Mamlaka ya usafiri wa reli TRC inasema itaanza kutoa huduma hiyo kwa ukamilifu kufikia mwezi Julai. #Kurunzi
Mpango wenye utata wa serikali ya Uingereza wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda hatimaye umeidhinishwa na Bunge mapema siku ya Jumanne.