Deutsche Welle: Watu 16 wauwawa kwenye machafuko ya kikabili na kidini nchini Nigeria huku mgomo wa nchi nzima ukiingia siku yake ya tatu leo.
Sikiliza Taarifa ya Habari asubuhi ya leo hapa
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anatazamiwa kukutana leo Jumatano na Kansela Olaf Scholz nchini Ujerumani. Baraza la Seneti la Marekani laidhinisha msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine, Israel na Taiwan. Ujumbe wa Mawaziri wa Korea Kaskazini wameanza ziara ya nadra nchini Iran.
Mpango wa Uingereza kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda waidhinishwa na Bunge. Rais wa Poland asema nchi yake iko tayari kupokea na kuhifadhi silaha za nyuklia za NATO. Viongozi wa Afrika watoa wito wa ushirikiano ili kupambana na ugaidi barani humo.