1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

14 wahukumiwa kwa shambulizi la Charlie Hebdo

Sudi Mnette
17 Desemba 2020

Mahakama nchini Ufaransa umewahukumu watu 14 hukumu ya kifungo cha kati ya miaka 4 hadi maisha gerezani kwa kuhusishwa na shambulizi la kigaidi la 2015 la jarida la tashtiti la Charlie Hebdo.

https://p.dw.com/p/3mq6I
Frankreich I Messerattacke in Paris
Picha: Alain Jocard/AFP/Getty Images

Miongoni mwa 14 hao yupo alietajwa kuwa mshitakiwa mkuu Ali Riza Polat, ambaye amekutwa na makosa ya kupanga mashambulizi hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani. Kijana wa umri wa miaka 35, mwenye asili ya Kifaransa na Kituruki amekutwa na hatia ya kusaidia na kuchochea uhalifu wenye dhamira ya kigaidi ikiwa ni miongoni na mashitaka mengine, pia amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.

Polat, ambae mara zote amekuwa akikanusha tuhuma hizo alisikika wakati wa hukumu akisema kwa sauti kwamba hicho kilichosemwa ni uongo. Lakini wote hao walikuwa katika mashtaka hayo walihusishwa kwa kutoa misaada kwa wahalifu kwa kuwapa misaada au vifaa kama gari. Aidha katika hukumu hiyo pia, mahakama iliyatupilia mbali mashtaka kadhaa dhidi ya watuhumiwa ambayo yaliwasilishwa na waendesha mashtaka.

Watuhumiwa watatu wahukumiwa bila ya kuwepo mahakamani

Hukumu hiyo inawahusu pia watuhumiwa watatu ambao inadaiwa walikimbilia katika mamlaka ya Kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kufanyika kwa tukio hilo la mauwaji la Paris, ambapo watu 17 walipoteza maisha.

Frankreich I Messerattacke in Paris
Waokozi wa Ufaransa wakimsaidia majeruhiPicha: Alain Jocard/AFP/Getty Images

Kwa mujibu ya wachunguzi nchini Ufaransa zipo hisia za ndugu wawili miongoni mwa watatu hao Mohammed na Mehdi Belhoucine wamekufa ingawa Mohammed alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Richard Malka, mwanasheria anaeliwakilisha jarida la Charlie Hebdo alisema "Kinachonivutia ni kwamba, ujumbe umetolewa kwa jamii na ujumbe huu ni kwamba yeyote atakaewasaidia magaidi kwa namna moja au nyingine atakabiliwa na hukumu kali."

Ali Riza anatazwamwa kama mtu wa karibu sana na muuaji Amedy Coulibaly

Kwa kuzingatia hukumu iliyotolewa, kituo kimoja cha radio cha umma cha France International, kimemnukuu mtoa hukumu, Jaji Mfawidhi Regis de Jorna akisema "Mahakama imegundua Polat alishiriki kwa kiwango kikubwa na kwa namna ya kimfumo kufanya uovu."

Soma zaidi: Kesi ya shambulizi la Charlie Hebdo yaanza kusikilizwa

Lakini hata hivyo wengi wa hao wameshindwa kujiepusha na mashtaka ya kushiriki biashara haramu ya silaha na dawa za kulevya. Polat anatazamwa kama mtu wa karibu sana na muuaji Amedy Coulibaly, ambaye alimuuwa polisi kwa kumpiga alimpiga risasi na baadae kuwauwa watu wanne waliochukuliwa mateka katika duka kubwa baada ya shambulio kwenye jarida hilo la Charlie Hebdo ambalo kwa wakati huo liliingia katika lawama kwa kuchapisha katuni zinazomdhihaki mtume Mohammed.

Hata hivyo Coulibaly aliuawa na polisi ambao walivamia na kulishambulia duka la vyakula ambalo ilihisiwa alikuwemo katika mkasa huo wa 2015.

Soma Zaidi:Charlie Hebdo latoa toleo jipya baada ya mauaji 

Chanzo/DPA