DeutscheWelle:timu zote 2 za Manchester zimewika ugenini katika duru za mchujo za ligi ya Ulaya,hali inayowapa moyo baada ya kutolewa katika kombe la vilabu bingwa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekataa kuidhinisha azimio la kuipatia Palestina uwanachama kamili baada ya Marekani kutumia kura yake ya turufu kuzuia azimio hilo
Wasiwasi wa kimataifa umeongezeka baada ya Israel kufanya mashambulizi ya droni nchini Iran+++Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa tajiri duniani ya G7 wamezungumzia wasiwasi wao kwa makampuni ya China juu ya kusafirisha vifaa vya kijeshi+++Hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mbaya zaidi na imepuuzwa zaidi katika historia ya ulimwengu
Duru zinasema Israel imefanya shambulio katika ardhi ya Iran mapema leo Ijumaa, siku kadhaa baada ya Iran kuishambulia kwa makombora na droni nchi hiyo katika hatua ya kulipiza kisasi. Hatua hiyo imezidisha wasiwasi wa kutanuka kwa mzozo katika kanda ya Mashariki ya Kati. #kurunzi