1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

2007 mwaka wa joto sana Ujerumani

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjSq

BERLIN:

Mwaka uliomalizika wa 2007 umekuwa mwaka wa joto zaidi kuliko yote nchini Ujerumani.

Kwa wastani hali ya joto nchini Ujerumani ,mnamo mwaka wa 2007 ,ilifikia rikodi mpya ya nyuzi-joto 9.80.Hii inaufanya mwaka huo kuwa mwaka wa joto zaidi kuliko yote tangu wanasayansi wa Kijerumani walipoanza kunukuu ujoto mwaka wa 1901.Maenedeleo kama hayo yanaweza kuchunguzwa katika nchi zingine za Ulaya kama vile-Austria na Uholanzi ambako hali ya joto kwa wastani ilifikia viwango vya juu mwaka wa 2007.Wanasayansi wa Uholanzi mabao nyaraka zao kuhusu hali ya hewa ndio nzee kuliko zote wanasema hii ni alama ya kuongezeka kwa ujoto duniani.