Timu ya kandanda ya Ujerumani, Bayern Munich, itakwenda Japan mwezi Mei mwaka huu kucheza mechi ya kuwasaidia wahanga wa zilzala na tsunami
Maafisa wa hospitali ya Palestina wamesema mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Israel usiku kucha katika mji wa Kusini wa Rafah, yamewauwa watu watano miongoni mwao watoto wawili wadogo.
Marekani inaharakisha kutuma silaha na vifaa vingine vya kivita nchini Ukraine, baada ya Rais Joe Biden kutia saini muswada uliocheleweshwa kwa muda mrefu wa kuiunga mkono nchi hiyo.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema kuna mkwamo katika mstari wa mbele wa mapambano ya Ukraine na kwamba hali hiyo inaruhusu kuanza kwa mazungumzo ya amani.