Deutsche Welle: Katika mechi za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika hivi leo, Sudan inakwaana na Burkina Faso, wakati Cote d'Ivoire ikitoana jasho na Angola.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema inasikitishwa na uamuzi wa Burkina Faso wa kuwafukuza wanadiplomasia na baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Ufaransa kutoka taifa hilo la Afrika Magharibi.
Serikali ya Burkina Faso imewafukuza wanadiplomasia watatu wa Ufaransa kutoka nchini humo ikiwatuhumu kuhusika na kile ilichosema ni "shughuli za uasi".
Watu 27 wameuawa katika shambulizi kwenye kijiji kimoja nchini Burkina Faso, wakiwemo wanawake na watoto.