1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

4 wafa na wengi kujeruhiwa wakati Polisi ya Kenya ikipambana dhidi ya waandamanaji

17 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cr6v

NAIROBI:

Polisi nchini Kenya imepambana na mamia ya waandamanaji wanaopinga uchaguzi uliomrejesha madarakani rais Mwai Kibaki katika siku ya kwanza ya msururu wa maandamano yaliyoitishwa na chama cha ODM.Maandamano hayo ambayo yalianza jana yalipangwa kueendelea kwa siku tatu. Siku ya pili ikiwa imeanza leo haijulikanai itakuwa je.Lakini katika siku ya kwanza mapambano makali kati ya polisi wa kuzuia fujo na waandamanaji yalitokea Kisumu ambako ni ngome ya Raila Odinga.Kuna taarifa za watu watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.Hatua ambayo imelaniwa na Raila Odinga .

Yeye waziri wa mashauri ya kigeni wa Kenya Moses Wetangula amesema kuwa maandamano hayo ni dhihirisho la ukaidi wa ODM usiofaa.

Watu zaidi ya 600 wameuawa katika ghasia za kisiasa ambazo zilianza baada ya kutokea sintofahamu ya matokeo ya uchaguzi wa mwezi jana.

Kwa mda huohuo Umoja waMatifa umetoa mwito wa haraka kwa mataifa anachama kutoa msaada wa kiutu wenye thamani ya Euro zipatazo millioni 28, kuwasaidia watu wanaokadiriwa kufika nusu millioni ambao wameathirika na ghasia za Kenya.Mapema muungano wa Ulaya ulisema kuwa utazuia misaada yake yote kwa serikali ya Kenya ikiwa mgogoro wa kiuchaguzi hautapatiwa ufumbuzi.