1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

58 wauwa katika ajali ya treni Pakistan

Siraj Kalyango20 Desemba 2007

Wengine 200 wajeruhiwa

https://p.dw.com/p/CdaQ
Waokoaji wa Pakistan wakitafuta maiti pamoja na majeruhi wa ajali ya treni karibu na Mehrabpur umbali wa kilomita 400 kaskazini mwa mji wa Karachi Jumatano, Dec. 19, 2007. Wengi wa abiria walikuwa wanakwenda kwa likizo ya Eid Al Adhha.Picha: AP

Watu wasiopungua 58 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa nchini Pakistan katika ajali ya gari moshi la abiria lililokuwa na abiria wengi wakiwa wanakwenda kwa likizo.

Ajali hiyo imetokea mapema alfajiri karibu na mji wa Mehrabpur,ulio umbali wa kilomita 300 kaskazini mwa mji wa Karachi.Na ilikuwa njiani kueleka Lahore.

Maafisa wanasema ajali ilitokea wakati mabehewa mengi ya garimoshi hilo la Karachi Express,yalipoacha njia na kuanza kugongana na baadae kuanguka.Afisa wa ngazi za juu wa shirika la reli nchini Pakistan amenukuliwa akisema kuwa ajali ilisababishwa tu na tatizo la kiufundi na wala sio mizengwe.

Kazi za uokozi zikishikishwa na raia na wanajeshi baado zinaendelea.

Waokoaji wamekuwa wakijaribu kuwafikia abiria waliokuwa baado wamenaswa katika mabehewa mawili kwa mda mrefu na ambayo yalikuwa yamebondekabondeka.Inaarifiwa watu 58 ndio wamefariki. Maafisa wa reli wanasema idadi ya vifo inaweza ikaongezeka.

Eneo la ajali limekuwa lijaa Mizigo, magurudumu ya reli pamoja na mabehewa mengine yaliyoharibiwa.

Wanajeshi kutoka kambi ya karibu walikuwa wanatumia machela kuwabeba waliojeruhiwa huku raia wa kawaida wakiendelea kukusanyika mahalai pa ajali.

Afisa moja wa shirika moja la utoaji wa huduma za dharura la Edhi-Anwar Kazmi ameeleza wandishi habari kuwa wakati huo idadi ya waliofariki ilikuwa 58 na majeruhi 122 na 40 kati yao ni mahtuti.hata hivyo kumekuwa na habari za kutatanisha kuhusu idaid ya wahanga huku baadhi ya wakuu kutoa idadi ya chini.

Wengi wa abiria walikuwa wakienda katika likizo ya waumini wa Kiilslam ya Eid al Adhha.

Maafisa wa kijeshi na reli nchini humo wanasema hajagundua chanzo cha ajali yenyewe ingawa meneja wa mtandao wa shirika la reli la Pakistan-. Asad Saeed, amesema huenda viunganisho katika reli ndio viliacha kwani hufanya hivyo wakati wa majira ya baridi.

Abiria moja ameripotiwa kusikia sauti ya ngurumo kabla ya ajali kutokea.

Afisa mwingine wa reli amesema kuwa mabehewa 14 katia ya yote 18 yaliacha njia na kuanguka na manne kati ya hayo yameharibika vibaya sana.

Ajali kama hiyo ilitokea mwaka wa 2005 wakati treni ya abiria,iliokuwa imejaa kupindukia, kugongana na nyingine katika kituo cha reli katika mkoa wa Sindh na kuwauwa watu 130.