1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas Kubaff azindua albamu yake Cologne

5 Aprili 2011

Mwanamuziki wa miondoko ya "Hip Hop" Abbas Kubaff, alizindua albamu yake mpya Jumamosi iliyopita jijini Cologne, Ujerumani. Mashabiki wengi walijirusha wakati mwanamuziki huyo maarufu kutoka Kenya alipowatumbuiza!

https://p.dw.com/p/RFX7

Mbali na kuwaburudisha mashibiki, muziki wa msanii Abbas Kubaff pia unatoa ujumbe unaohusu masuala ya jamii. Katika nyimbo zake, Kubaff anawashauri Waafrika wawe na umoja hata kama wanasiasa wakijaribu kuwatenga. Pia anawaasa vijana, wapatapo fedha wasizitumie bila kufikiria ila waweke akiba benki kwa ajili ya wakati wa baadaye.

Msanii huyo pia anatumia ziara yake barani Ulaya kwa ajili ya kuendeleza utalii baina ya bara la Afrika na Ulaya. Katika ziara ya kuizindua albamu yake inayobeba jina la "KBF 254" Kubaff atatembelea miji mbali mbali nchini Ujerumani na Uswisi.

Mwandishi: Elizabeth Shoo

Mhariri: Josephat Charo