1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abidjan. Muasi wa zamani awa waziri mkuu.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCQ

Nchini Ivory Coast , Guillaume Soro ameapishwa kuwa waziri mkuu. Kiongozi huyo wa zamani wa waasi , ambaye alikuwa anadhibiti eneo la kaskazini ya nchi hiyo kwa muda wa miaka minne, amesema umuhimu wa juu utakuwa katika kuchangia katika kupatikana kwa amani ya kudumu.

Anaingia madarakani kama sehemu ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa katika nchi jirani ya Burkina Fasso mwezi uliopita.

Jaribio lililoshindwa la Soro la kuipindua serikali ya rais Laurent Gbagbo miaka mitano iliyopita lilizusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Majeshi ya moja wa mataifa ya kulinda amani pamoja na yale ya Ufaransa yanashika doria hivi sasa katika eneo la kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili.