1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN : Rais Gbagbo amtangaza Soro kuwa waziri mkuu

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEL

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast amemtangaza rasmi kiongozi wa waasi Guilaume Soro kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.

Hii ni hatua mpya katika utekelezaji wa makubaliano ya amani ya kuiunganisha tena nchi hiyo yaliotiwa saini mapema mwezi huu nchini Burkina Faso kati ya Ghabgo na Soro.

Makubaliano hayo yaliosasisiwa na Waafrika wenyewe yamekuja baada ya makubaliano kadhaa yaliokuwa yakiungwa mkono na wageni kusambaratika na yanatazamia kuundwa kwa serikali mpya ya mpito ifikapo tarehe 8 mwezi wa April kuchukuwa nafasi ya serikali iliokuwa ikiungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya Waziri Mkuu Charles Konan Banny.

Soro aliongoza jaribio la mapinduzi lililoshindwa dhidi ya Gbagbo hapo mwaka 2002 na kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ambapo waasi walikuja kushikilia eneo la kaskazini na vikosi vya serikali vikidhibiti eneo la kusini.