1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN: Waasi nchini Ivory Coast wapinga muda zaidi madarakani kwa rais Laurent Gbagbo

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1Q

Waasi wanalolidhibiti eneo la kaskazini mwa Ivory Coast, wametupilia mbali pendekezo la Umoja wa Afrika kumuongezea muda wa mwaka moja zaidi madarakani rais Laurent Gbagbo.

Viongozi wa waasi wanasema pendekezo hilo ni kikwazo kwa juhudi za kutafuta amani. Maagizo ya Umoja wa Afrika yanatarajiwa kufikishwa mbele ya Baraza la usalama la Umoja wa mataifa wiki ijao ili kuidhinishwa. Inatarajiwa pia kuwa waziri mkuu Charles Konan Banny atapewa mamlaka zaidi. Kulikuwa kumepangwa kufanyika uchaguzi mkuu nchini Ivory Coast ifikapo tarehe 31 mwezi huu lakini uliahirishwa kutokana na mfarakano unaondelea kati ya serikali ya rais Laurent Gbagbo inaolidhibiti eneo la kusini na muungano wa makundi ya waasi wanaoidhibiti sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo.