1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN:Rais wa Ivory Coast ataka uchaguzi haraka kumaliza mzozo wa kisiasa

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbQ

Rais Laurent Gbabo wa Ivory Coast amesema kuwa serikali yake kwa sasa inaweza kuandaa uchaguzi mkuu ambao umeahirishwa mara mbili, itakapofika mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza katika mkesha wa siku ya uhuru wa nchi hiyo, Rais Gbabo amesema kuwa umefika wakati sasa wa kuondokana na mizozo ya kisiasa nchini humo kwa kuitisha uchaguzi mkuu.

Ivory Coast imegawika katika vipande viwili toka waasi walipotwaa eneo la kaskazini takriban miaka mitano iliyopita.

Rais Gbabo amemuelekeza Waziri Mkuu wa serikali ya mseto ambaye ni kiongozi wa waasi hao Guillaume Soro kufanya kila liwezekanalo ili uchaguzi huo ufanyike haraka.