1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABU DHABI.Kansela Angela Merkel awasili Abu Dhabi

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUl

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewasili katika umoja wa milki za kiarabu.

Huo ni mkondo wa tatu katika ziara yake ya siku nne huko mashariki ya kati.

Ujerumani ikiwa ndio mwenyekiti wa umoja wa ulaya inatarajiwa kufufua mpango wa amani wa mashariki ya kati na wakati huo huo kulijadili swala la mpango wa nyuklia wa Iran.

Kansela Merkel yuko mjini Abu Dhabi baada ya kukamilisha ziara yake huko Saudi Arabia ambako alifanya mazungumzo na mfalme Abdullah na mafisa wa ngazi za juu mjini Riyadh.

Mfalme Abdullah ameukosoa msimamo wa Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia, amesema kwamba msimamo wa Tehran ni wa makosa ijapo kuwa Saudi Arabia bado ni rafiki wa Iran.