1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABU DHABI:Kansela Merkel azilaumu Syria na Iran

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUf

Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel amezilaumu Syria na Iran kwa siasa zao katika mashariki ya kati na amezitaka nchi zote kutumia fursa iliyopo sasa ili kuleta suluhisho katika mgogoro baina ya Waisraeli na Wapalestina.

Kansela Merkel amesema katika hotuba aliyotoa mjini ABU DHABI kuwa Syria na Iran hazitaki kuona mafanikio katika juhudi za kuleta amani katika mashariki ya kati. Kiongozi huyo wa Ujerumani anaefanya ziara ya siku nne mashariki ya kati pia ameilaumu Iran kwa mpango wake wa nyuklia na sera za nchi hiyo nchini Lebanon.