1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Afrika kupambana na njaa

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClh

Viongozi wa nchi za Kiafrika hapo jana wamekubaliana juu ya mpango mpya wa utekelezaji kupambana na njaa ikiwa ni mfululizo wa maazimio kadhaa yaliotolewa hivi karibuni kabisa kupunguza tatizo la ukosefu wa usalama wa chakula katika bara hilo la kimaskini kabisa duniani.

Afrika haikupiga hatua kubwa za maendeleo katika kuboresha kiwango na ubora wa mazao yake na asilimia 27 ya Waafrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula ulio sugu licha ya kuwa na mikutano kadhaa ya viongozi na kupitisha maazimio ya kupambana na tatizo hilo.

Baada ya siku nne za mazungumzo ya waatalamu mabingwa na mawaziri katika mji mkuu wa Abuja nchini Nigeria wakuu wa nchi wameidhinisha mapendekezo ya kuongeza biashara kati ya mataifa ya Afrika,kuwekeza zaidi katika kilimo, kuboresha miundo mbinu na kutanuwa mpango wa kuwalisha watoto mashuleni.