1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Mateka waachiliwa huru.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwU

Wafanyakazi wanne raia wa Marekani wanaofanyakazi katika kisima cha mafuta waliotekwa nyara wiki kadha zilizopita katika jimbo la kusini nchini Nigeria wamekabidhiwa rasmi kwa maafisa.

Haijafahamika ni kwanini mateka hao wameachiliwa huru na maafisa wa ubalozi wa Marekani hawakuweza kupatikana kutoa maelezo.

Kwingineko nchini Nigeria waandamanaji wamekizingira kituo kimoja cha udhibiti wa bomba la mafuta kinachopeleka mafuta katika kituo cha kampuni la Royal Dutch Shell nchini humo, na kulazimisha kampuni hilo kusitisha mauzo yake ya nje ya kila siku ya mapipa 150,000 ya mafuta ghafi.