1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Ndege yaanguka na kuuwa abiria wote.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxy

Ndege moja ya Nigeria ikiwa na abiria wapatao 100 imeanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Ndege hiyo imeripotiwa kuwa ilikuwa inaelekea katika mji wa kaskazini wa Sokoto.

Inahofiwa kuwa abiria wote katika ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la binafsi la ADC wamekufa.