1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA: Nigeria ni bingwa wa kike wa kandanda barani Afrika

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtL

Timu ya soka ya wanawake ya Nigeria,imejinyakulia ubingwa wa kandanda wa wanawake barani Afrika kwa mara ya tano kwa mfululizo.Katika mechi ya fainali iliyochezwa Warri,wenyeji Nigeria waliikandika Ghana bao moja kwa bila.Nafasi ya tatu imechukuliwa na Afrika ya Kusini baada ya kupiga mabao ya penalti na kuipachika Kamerun magoli 5-4.Ushindi wa Nigeria na Ghana umezipatia nchi hizo tikti za kwenda kwenye mchuano wa Ubingwa wa Dunia.Mashindano hayo yatakuwa mwaka 2007 nchini China.