1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Upinzani walalamikia uchaguzi wa rais

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC84

Kura zimeanza kuhesabiwa nchini Nigeria wakati vyama vya upinzani vikilalamikia uchaguzi wa urais uliofanyika hapo jana ambao umetiwa dosari na umwagaji damu,mparaganyiko na kuchelewa kusambazwa kwa visanduku vya kupigia kura.

Makamo wa Rais Atiku Abubakar ameuelezea uchaguzi huo kuwa ni msiba wa taifa.Mwangalizi mmoja wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya nchini Nigeria amesema ana mashaka mazito juu ya uchaguzi huo.Kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo washambuliaji waliliendesha gari la mafuta kwenye makao makuu ya uchaguzi lakini gari hilo limeshindwa kuripuka.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi inapiga kura kumchaguwa mtu wa kurithi nafasi ya Rais Olusegun Obasanjo katika uchaguzi wa kwanza wa kiraia utakaokabidhi madaraka kwa serikali nyengine ya kiraia tokea uhuru wa nchi hiyo hapo mwaka 1960.