1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Vyama vya upinzani kushiriki sasa uchaguzi.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8m

Vyama vikuu vya upinzani nchini Nigeria vimesema kuwa vitashiriki katika uchaguzi wa rais kesho Jumamosi. Vyama viwili vikuu vya upinzani nchini Nigeria, All Nigeria Peoples Party ANPP, na Action Congress AC, vimesema kuwa vinaondoa tishio lao la hapo kabla la kususia uchaguzi huo.

Vyama hivyo viwili vilikuwa miongoni mwa vyama 18 ambavyo vilitishia kususia uchaguzi huo ambao ni wa kumtafuta mtu atakayechukua nafasi inayoachwa wazi na rais wa sasa Olusegun Obasanjo.

Mpambano wa uchaguzi huo utakuwa kati ya wagombea watatu maarufu , Umaru Yar’Adua wa chama tawala cha Peoples Democratic PDP, makamu wa rais Atiku Abubakar na mtawala wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari.