1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja. Wapinzani wapanga maandamano.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC72

Kundi moja la vyama vya upinzani nchini Nigeria limewataka wafuasi wake kuingia mitaani katika maandamano ya amani dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumamosi iliyopita.

Wachunguzi wa kimataifa na wa ndani wameukosoa uchaguzi huo na kusema kuwa ulikuwa na mapungufu mengi ambapo hauwezi kuelezwa kuwa una uhalali, na viongozi wa upinzani wanasema matokeo yake yabatilishwe.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi, uchaguzi huo umekwenda kwa ushindi wa kishindo kwa mgombea wa chama tawala , Umaru Yar’Adua.