1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Wito wa kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7w

Vyama vikuu vya upinzani nchini Nigeria leo hii vimeshutumu uchaguzi wa rais nchini Nigeria wakati kundi mashuhuri la waangalizi wa uchaguzi nchini humo limetowa wito wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo ambao ulikuwa umekusudia kuimarisha utawala wa kiraia.

Kundi la Hilo la Mpito la Kuangalia Uchaguzi lenye Wanigeria w 50,000 waangalizi wa uchaguzi limesema uchaguzi huo hakufanyika kwenye majimbo mengi kati ya majimbo 36 ya nchi hiyo na kwamba umechelewa sana kuanza katika majimbo mengi.Mwenyekiti wa kundi hilo Innocent Chukwuma amesema hiyo ndio sababu ya kutaka zoezi hilo zima la uchaguzi lifutwe.

Uchaguzi huo wa jana ulitiwa dosari na uhabawa na makaratasi ya kupigia kura katika ngome kuu za upinzani, vitisho vya wahuni na udanganyifu wa wazi unaoipendelea chama tawala.

Hata hivyo vya viwili vikuu vya upinzani havikusema kwamba vinaukata uchaguzi huo moja kwa moja na kwamba vinasubiri matokeo kutoka nchi nzima.

Msemaji wa chama cha Makamo wa Rais Atiku Abubakar amesema chama hicho yumkini kikapinga matokeo ya uchaguzi huo mahkamani.