1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA.Kura zaanza kuhesabiwa nchini Nigeria

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC86

Kura zimeanza kuhesabiwa katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria licha ya ghasia na vurumai zilizoutia dosari uchaguzi huo wa kihistoria.

Watoto watatu walipigwa risasi na kuuawa na wanajeshi katika mji wa Daura kaskazini mwa Nigeria. Watoto hao waliuawa wakati watu walipokuwa wanapinga walichodai kuwa ni wizi wa kura.

Watu wengine walijeruhiwa , baada ya wanajeshi kuwashambulia watu wanaounga mkono vyama vya upinzani.

Pia palikuwa na jaribio la kulipua makao makuu ya shughuli za uchaguzi.

Hatahivyo vituo vya kupigia kura vimefungwa na kura zimeanza kuhesabiwa katika uchaguzi huo ambapo wajumbe 24 wanagombea wadhifa wa urais.