1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA.Mateka waachiliwa huru

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSX

Mateka wote 24 waliotekwa nyara katika eneo la Delta ya Niger nchini Nigeria wameachiliwa huru.

Mateka hao raia wa Ufilipino walikuwa mabaharia katika meli ya kampuni moja ya Kijerumani Baco Liner walishikiliwa mateka tangu Januari 20.

Taarifa kutoka kwenye kampuni hiyo ya meli zimethibitisha kuwa mabaharia hao 24 wameachiliwa huru.