1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abuja.Olusegun Obasanjo atangaza hali ya hatari huko Ekiti.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1D

Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo, ametangaza hali ya hatari katika Jimbo la kusini magharibi mwa mji wa Ekiti, kufuatia, kile alichokiita kuwa kungolewa madarakani kwa Gavana kinyume na sheria.

Obasanjo amemteuwa Meja Jenerali mstaafu kusimamia shughuli za jimbo hilo.

Wabunge wiki hii walipiga kura ya kuondoshwa Gavana Ayo Fayose baada ya kupatikana na hatia ya kuhamishia fedha za serikali katika akaunti yake binafsi.

Nigeria nchi ambayo ina wakaazi wengi barani Afrika, inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi April mwakani utakaofungua njia ya kuelekea katika demokrasia tangu kupata uhuru mwaka 1960.