1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Accra. Rais wa Ujerumani afungua mkutano wa ushirikiano na Afrika

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaq
Mawasiliano kwa njia ya mtandao.
Mawasiliano kwa njia ya mtandao.Picha: picture-alliance/dpa

.

Rais wa Ujerumani Horst Köhler ambaye yuko katika ziara ya siku nne nchini Ghana, ametoa wito kwa umoja wa Ulaya kubadili mtazamo wake kuielekea Afrika.

Akihutubia kikao cha ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kuhusu uhusiano kati ya Ujerumani na mataifa ya Afrika, pia ameshutumu kile alichokiita vitendo vya ulaji rushwa vinavyofanywa na baadhi ya makampuni ya Ujerumani katika Afrika.

Köhler amelitaka bara la Ulaya kutoinyima Afrika nafasi ya kuuza bidhaa zake na hususan alielezea athari mbaya za sera za uvuvi za umoja wa Ulaya.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za Köhler za ushirikiano na Afrika. Mkutano wa kwanza wa kama huo ulifanyika Novemba 2005 karibu na Bonn.