1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Rais wa Ujerumani ziarani Ghana

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbI

Rais wa Ujerumani Hörst Kohler ameyataka mataifa ya Afrika yashirikiane na Ulaya kuzipiga jeki juhudi za kutafuta amani nchini Somalia na maeneo mengine ya mizozo barani Afrika.

Rais Köhler amesema Ujerumani inaweza kushirikiana na taifa kama Ghana kuongeza juhudi za kurejedha utulivu Somalia na maeneo mengine ya vita. aidha rais Köhler amesema nchini yake itaendelea kuisaidia Ghana katika jukumu lake la kuongoza juhudi za kulinda amani.

Ameeleza kuridhika kwake kwa Ghana kufanya mafunzo ya kulinda amani yaliyodhaminiwa na Ujerumani na kasema sasa itaweza kupeleka majeshi yake kushiriki katika vikosi vya kimataifa vya kulinda amani.