1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Accra. Viongozi waanza mkutano.

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmw

Viongozi wa umoja wa Afrika wanaanza mkutano wao wa siku tatu leo Jumapili utakaolenga katika mipango ya kuunda shirikisho la mataifa hayo ambalo litasaidia bara hilo masikini sana kuwa na nguvu katika medani ya kimataifa.

Polisi na wanajeshi walijipanga katika mitaa ya mji mkuu wa Ghana wakati viongozi hao walipokuwa wakiwasili kwa ajili ya mkutano huo, ukiwa ni wa tisa tangu kuundwa kwa umoja huo miaka mitano iliyopita.

Wakati huo huo rais Omar al-Bashir wa Sudan jana ameyaonya mataifa ya magharibi kutovuruga ushughulikiaji wa mzozo katika jimbo lenye matatizo nchini humo la Darfur kama ilivyofanya nchini Iraq.

Akizungumza na waandishi wa habari kupitia satalaiti kutoka mjini Khartoum, Bashir, ambaye hakuhudhuria mkutano wa mataifa ya umoja wa Afrika kutokana na kifo cha mshauri wake wa karibu kilichosababishwa na ajali ya gari, amesema kuwa mataifa ya magharibi yameutia chunvi mno mzozo wa Darfur kwasababu ya maslahi yao katika hifadhi ya mafuta nchini humo.

Rais Bashir ambaye mara kwa mara anayashutumu mataifa ya magharibi kwa kutaka kuuangusha utawala wake, amesema kuwa Marekani inataka kufanya makosa yale yale iliyoyafanya nchini Iraq.