1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Waghana waadhimisha miaka 50 ya uhuru

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLn

Waghana wamejitokeza kwa wingi hii leo kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru kutoka kwa Uingereza.

Maelfu ya Waghana wamekusanyika katika uwanja wa uhuru mjini Accra, mahali ambapo kunafanyika magwaride ja kijeshi. Eneo hilo ni karibu na kiwanja cha Old Polo ambako Kwame Nkurumah, rais wa kwanza wa Ghana, alisherehekea uhuru kama waziri mkuu.

Uhuru wa Ghana uliyafungulia mlango mataifa mengine barani Afrika kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni.