1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACEH, INDONESIA: Mafuriiko yasababisha maafa Indonesia

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCft

Takriban watu mia moja na tisa wamefariki kutokana na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi.

Wafanyikazi wa kutoa misaada ya dharura wanaendelea na shughuli ya kutoa vyakula na makazi kwa watu takriban laki tatu na elfu tisini waliopoteza makazi yao kwa sababu ya mafuriko katika jimbo la Aceh, Indonesia.

Watu sabini wamefariki na wengine mia mbili wametoweka baada ya mafuriko kukumba kisiwa hicho mwisho.

Wafanyikazi wa afya wameanza kutia dawa maji ili kuzuia uwezekano wa kutokea maradhi ya kuambukiza.

Kiasi cha miaka miwili iliopita jimbo la Aceh lilikuwa miongoni mwa maeneo ya bara la Eshia yaliyokubwa na janga la Tsunami.