1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Serikali yawasiliana na wateka nyara

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKb

Serikali ya Ethiopia imekuwa na mawasiliano na wateka nyara wa kundi la watalii wa Ulaya.

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Seyoum Mesfin amewaambia waandishi wa habari leo hii kwamba wanaohusika na tukio hilo wamekuwa wakiwasiliana nao katika njia mbali mbali na kwamba wanataraji mateka hao wataachiliwa bila kudhuriwa.

Seyoum hakutowa ufafanuzi zaidi juu ya mawasiliano hayo isipokuwa amesema wahusika wako katika jimbo la Afar kadhalika amekataa kuzungumzia tetesi juu ya nchi wanakoshikiliwa mateka.

Kundi la wafanyakazi watano wa ubalozi wa Uingereza mjini Addis Ababa au jamaa zao walitekwa nyara pamoja na Waethiopia 13 ambo walikuwa ni madereva na wakalimani hapo tarehe Mosi mwezi wa Machi.

Wanne wa mateka hao inaaminika kuwa ni raia wa Uingereza na mmoja ni raia wa Ufaransa.