1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Ethiopia yatolewa wito kudumisha uhuru wa demokrasia

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IU

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anatoa wito kwa nchi ya Ethiopia kuruhusu uhuru wa demokrasia baada ya nchi hiyo kushtumiwa na jamii ya kimataifa kuhusu uchaguzi wa mwaka 2005. Bi Merkel na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi walijadilia ushirikiano,migogoro ya eneo hilo hususan jimbo la Darfur nchini Sudan pamoja na nchi jirani ya Somalia.Mzozo wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea pia ulikuwa katika ajenda ya mazungumzo hayo.

Bi Merkel yuko nchini Ethiopia ikiwa ni sehemu ya kwanza ya ziara yake barani Afrika inayotazamiwa kumpeleka katika mataifa ya Afrika Kusini na Liberia.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini Ethiopia walikamatwa na kuzuiliwa katika msako mkubwa kufuatia uchaguzi wa wabunge mwaka 2005 uliodaiwa kuwa na dosari.

Viongozi hao waliokabiliwa na kifungo cha kirefu jela waliachiwa mwezi Julai baada ya msamaha wa rais.

Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi ameahidi kupeleka majeshi alfu 5 kuchangia katika kikosi cha Umoja wa Mataifa na Afrika kinachopangw akupelekwa katika eneo la mzozo la Darfur.Kikosi hicho kiliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa mapmea mwaka huu na serikali ya Sudan imeridhia.