1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Kondomu za harufu ya kahawa kupambana na Ukimwi

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AV

Shirika moja la misaada la Marekani linaanzisha mpango wa kusambaza mipira ya kondomu iliyo na harufu ya kahawa.Mkakati huo unalenga kupambana na Ukimwi katika nchi iliyo na utamaduni wa kahawa.Ethiopia inakabiliwa na maambukizi ya ukimwi ya asilimia 2.1 huku eneo la mjini lilkiwa na asilimia 7.Kwa mujibu wa Andrew Piller mkuu wa tawi la Ethiopia la Shirika la DKT International lililo na makao yake mjini Washington linasema kuwa lengo la mipira hiyo ni kufanya matumizi yake kuwa bora zaidi wala sio kupata faida.

Shirika la DKT limebaini kuwa baadhi ya watumiaji wa mipira hiyo ya kondom wanalalamikia harufu ya kipira ya kondomu za kawaida.Jambo hilo limelifanya shirika hilo kutengeza bidhaa zinazoambatana na utamaduni wa nchi.

Kondomu laki tatu zinaripotiwa kununuliwa katika kipindi cha wiki moja mwezi wa Septemba nchini Ethiopia wakti ilipoanza kusambazwa.

Kondom hizo zinauzwa tatu kwa kila paketi kwa yapata senti 11.Kikombe kimoja cha kahawa nchini humo ni mara mbili ya kiwango hicho na bei hiyo ni chini zaidi kuliko kondom nyingine.