1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Adhabu ya kifo ya Misri yalaaniwa vikali

Admin.WagnerD29 Aprili 2014

Umoja wa Mataifa na Marekani wamelaani vikali adhabu ya kifo dhidi ya watu 683 wanaodaiwa kuwa ni waislamu wenye msimamo mkali akiiwemo kiongozi wa chama cha udugu wa Kiislamu Mohamed Badie.

https://p.dw.com/p/1BqfI
Ägypten Gerichtsurteil 28.04.2014 Minya
Baadhi ya raia wa MisriPicha: picture-alliance/dpa

Mahakama iliyopo katika jimbo la kusini la Minya ilizusha kilio kwa jumuiya ya kimataifa baada ya hukumu ya mwanzo ya kifo ya mwezi uliyopita, iliyotajwa kuwa ukandamizaji mkali kabisa dhidi ya wafuasi wa kiongozi mwenye itikadi kali Mohammed Mursi. Marekani imetaka Misri kubadili uamuzi wa mahakama. Taarifa ya Ikulu inasema umauzi huo umekwenda kinyume sheria za kimataifa za haki za binaadamu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy amesema uhusiano wa taifa lake na Marekani umeendelea kuwa mgumu na kwa hakika mazungumzo baina ya mataifa hayo mawili yanahitajika ili kurejesha uhusiano huo katika mstari mmoja.

Neu ernannter Außenminister Ägypten Nabil Fahmi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil FahmiPicha: STR/AFP/Getty Images

Akizungumza katika mkutano mmoja wa maafisa wa ngazi za juu mjini Washington waziri huyo amesema tofauti hiyo imekuwepo tangu kutokea mageuzi ya 2011 na hata baada ya jeshi kumuondoa madarakani kiongozi aliyechaguliwa kidemokrsia Mohammed Mursi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alitoa tahadhari kuwa hukumu hiyo inaweza kuleta athari hata nje ya mipaka ya Misri. Kwa mujibu wa msemaji Stephane Dujarric kiongozi huyo ameongeza kwa kusema uamuzi huo wa jumla jamala unaonesha dhahiri haujafikia viwango vya haki na hasa kwa kutolewa kwa adhabu ya vifo kunaongeza hofu ya kutokuwepo kwa utulivu kwa muda mrefu nchini humo.

Jitihada za Ban Ki-moon

Aidha amepanga kujadili masikitiko yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy baadae wiki hii. Mahakama ya Minya chini ya Jaji Said Youssef Sabri, imepanga kuthibitisha adhabu hiyo ifikapo Juni 21 mwaka huu. Vilevile imebadilisha uamuzi wa watuhumiwa 492 kati ya 529 waliohukimiwa adhabu ya kifo Machi, ambapo wengi wa hao wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Awali katika hatua nyingine mjini Cairo, mahakama moja Aprili 6 ilipiga marufuku harakati za vijana ambao walishiriki maandamano ya 2011 yaliomuondoa madarakani rais wa zamani wa taifa hilo Hosni Mubarak, kutokana na tuhuma za kuikashifu serikali ya Misri na kushirikiana na asasi za kigeni. Ban vilevilie ameonesha kusikitisha kwake na uamuzi huo ambao uliambapata na kuwafunga watu watatu muhimu waolishiriki katika vuguvugu la mwaka 2011 wakiwemo waasisi wawili wa harakati za vijana.

Wakili kutoka upande wa walalamikaji Khaled Elkomy ambae alikuwepo mahakamani hapo jana wakati uamuzi huo unatolewa alisema kesi hiyo ilisikilizwa kwa dakika kumi tu. Uamuzi huo ulikuwa wa kwanza kutolewa dhidi ya kiongozi wa kidini wa chama cha Udugu wa Kiislamu, Mohamed Badie ambae pia anakabiliwa na mashitiaka mengine yakiwemo yanayomuhusu rais Mursi.

Mwandishi: Sudi MnetteAFP
Mhariri:Yusuf Saumu