1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON yaanza na ukame wa mabao

Admin.WagnerD17 Januari 2017

Mabingwa watetezi kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Africa, AFCON Ivory Coast na Morocco, ambazo pia zina idadi kubwa ya mashabiki, Jumatatu hii zimeshindwa kuonyesha ubabe wao.

https://p.dw.com/p/2VuO7
Fußball Afrika-Cup Elfenbeinküste v Togo FBL-AFR-2017-MATCH05-CIV-TOG
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Jumatatu hii timu hizo zimeshindwa kuonyesha ubabe wao, baada ya Ivory Coast kutoka sare ya bila kufungana na Togo, huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ikiibwaga  Morocco, bao 1-0. 

Ivory Coast inayotetea kombe hilo, iliyotoka sare na Togo, ambayo inashika nafasi ya 21 ya viwango vya soka nyuma ya Ivory Coast, ilicheza kwa kiwango cha kawaida huku mechi hiyo ikikosa msisimko mbele ya mashabiki wachache waliojitokeza kwenye uwanja wa Stade d‘Oyem.

Morocco, ambayo pia inapewa nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo, chini ya kocha Herve Renard, aliyefanikisha kutwaa kombe hilo mwaka 2015 ilipigwa bao 1-0 na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.  Congo ambayo ilishinda kombe hilo kwa mara ya mwisho miaka 43 iliyopita, Inaongoza kundi C baada ya kujizolea pointi tatu katika raundi ya kwanza.

Ivory Coast na Togo wote zina pointi 1, huku Morocco  ambayo ilipata mafaniko makubwa kwenye michuano hiyo mwaka 1976, ikiwa haina pointi yoyote na inaburuta mkia kwenye kundi hilo.

Mechi nne kati ya sita kwenye michuano hiyo zimetoa droo, baada ya Cameroon kukamatwa na Burkina Faso , huku wenyeji Gabon ikitoka sare na Guinea Bissau na Algeria ikitoka sare na Zimbabwe.

Fußball Qualilfikation African Cup of Nation 2017 Pierre Aubameyang
Picha: Getty Images/AFP

Siku ya ufunguzi ilishuhudia, Guinnea Bissau na Burkinafaso zikipanda kwa kasi baada ya matokeo yasiyotarajiwa ya sare ya kutofungana dhidi ya Gabon na Cameroon, katika mechi za kundi A. 

Hata hivyo kocha wa Gabon Jose Antonio Camacho alisema ni heshima kubwa kuwa na mchezaji kama Pierre- Emerick Aubameyang katika michuano hiyo katika kujiweka katika nafasi ya kuendelea mbele kwenye michuano kama hiyo.

Aubameyang ameahidi kuiongoza vyema timu yake ambayo ni mwenyeji wa michuano hiyo, baada ya kuanza vibaya, wakati itakapokutana na Burkina Faso Jumatano hii kwenye raundi ya pili ya mechi za kundi A mjini Libreville .

Mechi nyingine za kundi A Jumatano  ni Cameroon dhidi ya Guinnea Bissau.


Mwandishi: Lilian Mtono.
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman