1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika hatari ya kukabiliwa na mizozo inayotokana na mgogoro wa kiuchumi duniani.

Jason Nyakundi11 Mei 2009

Uchumi wa nchi nyingi utazorota mwaka huu.

https://p.dw.com/p/Ho4P
Ölproduktion in Angola
Vituo vya mafuta nchini Angola.Picha: AP

Mgogoro wa kiuchumi uanaondelea kuikumba dunia hivi sasa umechangia zaidi katika hatari ya kutokea ghasia na mizozo barani afrika ambapo maendeleo yamepungua kutokana na kuzorota kwa uchumi katika mataifa tajiri. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD.

Shirika la OECD, Benki ya maendeleo barani Afrika pamoja na tume ya uchumi ya umoja wa mataifa kwa Afrika yameonya kuwa kuna ishara ya msuko suko wa kisiasa ambao hautapuuzwa

Kulingana na ripoti iliyotolewa na mashirika hayo ni kuwa maendeleo katika bara la Afrika yatapungua hadi asilimia 2.8 mwaka huu kutoka asilimia 5.8 mwaka uliopita.

Shirika la OECD linasema kuwa hali hii imesalia kuwa tete katika baadhi ya nchi na huenda ikawa mbaya zaidi katika miezi inayokuja kutokana na suala kuwa hali ya kiuchumi inazidi kuwa mbaya zaidi duniani.

Hata kama nchi kadha zilifanikiwa kukabiliana na hali hii mwaka 2008 kwa kuweka mikakati, hali hii itakuwa ni changamoto mwaka huu hasa baada ya kupungua kwa raslimali.

Uchumi wa nchi nne kati ya nchi 52 zilizofanyiwa utafiti utazorota zaidi.Angola ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta barani afrika uchumi wake utazota ktoka asilimia 15.8 mwaka uliopita hadi na kunyea dhadi asilimi 7.2 mwaka huu huku ule wa usheli sheli ukinywea kwa asilimia 0.4

Uchumi wa Jamuri ya kidemokrasi ya kongo utanywea kwa silimi 0.6 huku ule wa chad ukinywea kwa silimia 0.7. Jamhuri ya Afrika ya kati itaadhirika zaidi kutokana na mazozo wa kiuchumi uliopo sasa huku ikishuhudia asilimia 0.2 katika kuzorota kwa uchumi wake.

Afrika kusini, nchi iliyo na uchumi dhabiti zaidi barani Afrika itashuhudia kupungua kwa pato la jumla la nchi likipungua kutoka asilimia 3.1 mwaka uliopita hadi asilimia 1.1 mwaka huu.

Nchi nyingi barani Afrika tayari zimeshuhudia maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya vyakula kwa muda wa miezi 18 iliyopita huku pia mapinduzi ya kijeshi nchini Mauritania na Guinea yakitajwa.

Jeshi lilingilia kati na kusaidia kumpindua rais wa Madagascar mwaka huu huku jeshi pia likiimua rais nchini Gunea Bissau.

Shrika la OECD linasema kuwa hali nchini Somalia ni mbaya huku vita vya wenyewe kwa wenyewe sasa vikiingia mwaka wake wa 18 na ukosefu wa serikali dhabiti nchini Somalia sasa unatishia utulivu wa eneo hilo lote.

Nchini Cameroon kulifanyika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya vyakula pamoja na yale ya kupinga pia hatua ya rais Pual Biya ya kutaka kuifanyia katiba mabadiliko yatakayomruhusu kuwania awamu ya tatu kama rais wa nchi hiyo.

Hata hivyo hatua zilizochukuliwa na nchi hizi zilizaa matunda lakini tatizo hili litaendelea hasa kutokana na kupungua kwa raslimali na pia kutokana na ukosefu wa misaada.

Mwandishi : Jason Nyakundi/AFP

Mhariri : Mohammed AbdulRahman.