1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Abdu Said Mtullya25 Aprili 2014

Magazeti ya Ujerumani wiki hii yameandika juu ya hatari ya njaa Sudan kusini,na juu ya kutimuliwa kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokasi ya Kongo kutoka Kongo Brazzaville.

https://p.dw.com/p/1BocZ
Masahibu yanayowafika watu Sudan Kusini
Masahibu yanayowafika watu Sudan KusiniPicha: picture-alliance/AP Photo

Gazeti la "Süddeutsche" limeandika juu ya mgogoro wa Sudan Kusini.Gazeti hilo linatanabahisha katika makala yake kwamba watu wa nchihiyo wamo katika hatari kubwa ya kufa njaa kutokana na mapigano.

Gazeti hilo linaeleza kwamba kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan Kusini inaelekea kwenye maafa makubwa ya njaa. Gazeti hilo limemkariri mjumbe wa shirika la Misaada ya Chakula Duniani "Welthungehilfe" Jürgen Gihr akisema kwamba bomu la njaa linadunda katika Sudan Kusini na linakaribia kuripuka.

Mjumbe huyo amekaririwa akieleza kuwa ,kwa kawaida katika nyakati kama hizi wakulima wa nchi hiyo wangelikuwa wanapanda mbegu za mahindi,maharagwe, na mboga mboga kama nyanya na bamia. Lakini mnamo mwaka huu hali siyo ya kawaida hata kidogo. Ameeleza kuwa sasa ni miezi minne tokea majeshi ya serikali yaanze kupambana na wapigajani wa waasi.

Hatua za haraka zinahitajika kuwaokoa watu

Gazeti la "Süddeutsche" pia limemnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka. Ban Ki-moon amekakariwa akimesema kwamba, ikiwa hatua hizo hazitachukuliwa mara moja, watu hadi milioni moja watakufa njaa mnamo miezi michache ijayo katika Sudan Kusini.

Gazeti la "die tageszeitung" limeandika maoni juu ya hali ya Sudan Kusini na linasema kuwa hali ni mbaya sana katika nchi hiyo na kwa hivyo jumuiya ya kimataifa inapaswa iitilieamaanani nchi hiyo.

Wafukuzwa na jirani zao

Gazeti la "die tageszeitung" pia limechapisha makala juu ya "Mbata ya Mokolo"

Gazeti hilo linaeleza kwamba maalfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanaodaiwa kuishi katika Kongo Brazzaville kinyume na sheria wamefukuzwa nchini humo. Mpango wa polisi wa kuwakamata na kuwafukuza watu hao unaoitwa "Mbata ya Mokolo", ulianza kutekelezwa tokea tarehe tatu ya mwezi huu.Lakini gazeti la "die tageszeitung " limeripoti kwamba mpango huo uliandamana na matumizi ya nguvu.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti hilo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hadi alfu nane walimesharudishwa kwao kwa nguvu kutoka Kongo Brazaville tokea mwanzoni mwa mwezi wa Aprili.

Balozi athibitisha vifo vya watu watatu

Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika Kongo Brazzaville Christophe Muzungu amekaririwa akisema kwamba raia watatu wa nchi yake wamekufa kutokana na purukushani ya kuutekeleza mpango wa Mbata ya Mokolo .Walengwa ni wanawake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanaofanya kazi ya ukahaba kinyume na sheria katika Kongo Brazzaville.

Kwa mujibu wa gazeti la "die tageszeitung" serikali ya Kongo Brazzaville inalalamika kwamba raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanafanya vitendo vya kihalifu,kama wizi na ubakakaji nchini Kongo Brazzaville.

Mapenzi hayazeeki
Gazeti la "Die Zeit" limeripoti juu ya tabia ya wanawake "maajuza" wa Kijerumani wanaofanya mapenzi na vijana wa Kenya.

Gazeti hilo linatufahamsiha zaidi kwamba aghalabu umri kati ya pande mbili hizo unapishana kwa miaka hadi 30.Gazeti la "Die Zeit" limetoa mfano wa mama mmoja wa Kijerumani anaeitwa Birgit. Mama huyo mwenye umri wa miaka hamsini amefahamiana na kijana mmoja wa Kenya anaeitwa Sam mwenye umri wa miaka 20. Sama ni miongoni mwa vijana wa kigiriama wanaoitwa " Beachboys".


Mambo hayo yanatukia kwenye fukwe za kitalii katika jiji maarufu la Mombasa nchini Kenya. Vijana wa Kenya wanatumia msemo : ukipenda,chongo utaiita kengeza. Hata hivyo gazeti la "Die Zeit"linaeleza kwamba wakati wanawake wa kijerumani wanazungumzia juu ya mapenzi "Beach boys" wanazungumzia juu ya biashara. Hadithi yenye nyuso mbili kama mwezi Januari.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman