1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Abdu Said Mtullya20 Juni 2014

Magazeti ya Ujerumani wiki hii yameandika juu ya mashambulio ya kigaidi yaliyowalenga washabiki wa kandanda nchini Kenya na Nigeria, pia juu ya mapigano baina Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

https://p.dw.com/p/1CMzh
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo Martin Kobler akisalimiana na watoto
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo Martin Kobler akisalimiana na watotoPicha: DW/D. Köpp

Gazeti la "Die Welt"limeandika juu ya mashambulio yaliyofanywa na magaidi nchini Kenya na Nigeria. Magaidi hao wamewashambulia watu, waliokuwa wanaangalia mechi za mashindano ya Kombe la Dunia. Gazeti la "Die Welt" linaeleza kwamba magaidi hao waliwalenga hasa washabiki wa kandanda kwa sababu wanaichukia michezo kama vile wanavyochukia kila kitu kinachouashiria utamaduni wa magharibi.

Gazeti la "Die Welt" linaeleza kuwa mshambuliaji wa kujitoa muhanga alijiripua mahala ambapo watu walikusanyika katika jimbo la Yobe nchini Nigeria ili kuangalia mpira. Watu zaidi ya 20waliuawa kutokana na shambulio hilo.

Mpeketoni

Gazeti la "Die Welt" pia limeandika juu ya shambulio lingine la kigaidi lililofanyika kwenye kitongoji cha Mpeketoni katika jiji la Mombasa, Kenya. Watu 48 waliuawa kutokana na shambulio hilo. Hata hivyo, gazeti la "Die Welt" linasema Rais Uhuru Kenyatta aliwashangaza watu aliposema kuwa mitandao ya kisiasa ya ndani ya Kenya ndiyo iliyohusika na shambulio hilo.

Kongo na Rwanda ziwashana risasi

Gazeti la "Die Tageszeitung" wiki hii limeandika juu ya hali ya kutoaminiana iliyozuka tena baina ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Gazeti hilo linaeleza kwamba mapigano yaliripuka kati ya majeshi ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Kila nchi iliyaimarisha majeshi yake na mapigano yaliendelea kwa muda wa siku mbili wiki iliyopita. Kila upande unautupia lawama mwingine kwa kuyaanzisha mapigano hayo.

Rwanda inadai kwamba wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo walivuka mpaka na kuingia ndani ya Rwanda ambako walipora ng'ombe na kudai fedha kutoka kwa wakulima ili wawarudishe wanyama hao. Kwa upande wake Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imedai kwamba askari wa Rwanda walimteka nyara kanali mmoja wa Kongo, wakamtesa na baadaye kumuua. Wakati huo huo juhudi za kuleta amani zinafanyika. Gazeti la "die tageszeitung" linatilia maanani kwamba mkuu wa jeshi la kulinda amani nchini Kongo, Martin Kobler, alienda Rwanda kwa ajili ya mazungumzo ya kuleta amani.

NARR:
Gazeti la "die tageszeitung" linaeleza kuwa uhusiano baina ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ulianza kuwa mzuri baada ya kundi la waasi la M 23 kuamua kuziweka silaha chini mashariki mwa Kongo lakini gazeti hilo linasema kuwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inakataa kuwachukulia hatua wanamgambo wa kihutu wa kundi la FDLR waliopo nchini Kongo.Wanamgambo hao wanatuhumiwa na Rwanda kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994.

Gazeti la "Süddeutsche " wiki hii limeandika juu ya maradhi ya kupooza yanayowaathiri watoto duniani kote-Gazeti hilo linatilia maanani kwamba madaktari wanaziimarisha juhudi za kupambana na maradhi hayo lakini gazeti linasema juhudi hizo zinakabiliwa na vizingiti na linautoa mfano wa Nigeria.

NARR:
Harakati za kupambana na maradhi ya kupooza kwa watoto zimegeuzwa kuwa suala la kisiasa nchini Nigeria.Waislamu wenye itikadi kali kaskazini mwa nchi hiyo wanaeneza uzushi kwamba chanjo inayotolewa kwa watoto ni simu.

ABDU:
Gazeti la "Süddeutsche" linakumbusha kwamba mnamo mwaka wa 2003 nesi mmoja alipigwa risasi na magaidi wanaopinga chanjo hiyo kutolewa kwa watoto.Magaidi hao wanadai kwamba nchi za magharibi zinakusudia kuwaua watoto wa kiislamu kwa njia ya kuwapa sumu.

Naam , hadi hapo tunayakamilisha makala haya ya Afrika katika magazeti ya Ujerumani, Kwa niaba ya mwenzangu..... mimi ni am kutoka hapa Bonn.

Mwandishi: Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Khelef