1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini baada ya kifo cha Terre Blanche

9 Aprili 2010

Inaelekea wapi ?

https://p.dw.com/p/MrYL
Je, vipi usalama wa mashabiki wa kombe la dunia ?Picha: picture alliance / dpa

Nchini Afrika Kusini ,leo ni maziko ya Kiongozi wa kizungu aliekuwa na siasa kali za mrengo wa kulia Terre Blanche.Mazishi yake yanafanyika chini ya ulinzi mkali katika shamba lake kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ambako Jumamosi iliopita baada ya mabishano juu ya kutowalipa ujira wao wafanyikazi wake 2 wa kiafrika, alipigwa hadi kufa. Kuuwawa kwa Terre Blanche, kumechochea hali ya wasi wasi ambayo wiki 10 kabla firimbi kulia kuanzisha Kombe la Dunia, kumetandaza wingu lake juu ya anga la nchi hii mwenyeji.

Ni picha zisizopendeza zinazoenea ulimwenguni siku hizi kutoka Afrika kusini:Polisi wakijitahidi kijijini kuwatenganisha wazungu upande mmoja na waafrika upande wapili.Kundi moja likiimba "Waueni makaburu" na jengine wimbo wa Taifa wa enzi ya utawala wa ubaguzi na mtengano (Aparthied) "Die Stem".

Na hii ni mbaya kabisa ,kwavile, inakumbusha siku za maovu zilizopita. Kuna lakini tofauti moja: enzi za utawala wa ubaguzi na mtengano, Waandamanaji kama hao wa kiafrika wangetawanywa kwa kukandikwa risasi lakini leo , askari wa kizungu wanalinda haki zao za kutoa maoni yao haki inayohakikishwa na katiba ya Afrika kusini, mojawapo ya katiba zenye uhuru mkubwa ulimwenguni.Wakati huo huo, Mahkama ya Afrika kusini, inampiga marufuku Kiongozi wa chama cha vijana cha ANC kwimba nyimbo za kuieneza uchuki dhidi ya wakulima wa kizungu.

Ikiwa inawafikiana na vyombo vya habari ambavyo vinachora sura ya hofu ya kuzuka vita vya kikabila katika Ras ya Matumaini mema (Cape of good hope) au la, Afrika kusini tangu kupita miaka 16 sasa ya kuimalizika kwa utawala wa ubaguzi na mtengano-aparthied-imepiga hatua kubwa usoni.Kizazi kilichofuatia kuja kwa mzee Mandela kufuatia kutoweka kwa aparthied, hakijitambulishi tena chini ya misngi ya rangi,bali kinasherehekea katika madisco pamoja mjini Johannesberg.

Kabisa kabisa, matatizo ya Afrika Kusini, hayapo katika enzi zilizopita, bali ya wakati huu tulionao:Na yapo kwenye uongozi dhaifu wa kisiasa.

.....Ikiwa leo hii, mwaka tangu kun'gatuka wadhifa wa urais, waafrika kusini wanamtamani tena rais wa zamani Thabo Mbeki, basi si sifa nzuri kwa uongozi wa Jacob zuma na timu yake serikalini.Hivi sasa hata wapigakura wa ANC wananun'gunika....Ilikuaje Kiongozi huyo kumuachia Kiongozi wake wa chama cha vijana cha ANC, Julius Malema -mtu alieimba ule wimbo "waueni m akaburu" kwenda Zimbabwe, kumpongeza rais Mugabe na siasa zake za mageuzi ya ardhi wakati binafsi rais Zuma, alikwenda huko kupatanisha ?

Kwanini ilimchukua Zuma siku 4 tangu kuuwawa kwa Terre Blanche kumfunga mdomo asiimbe nyimbo hiyo,kitu ambacho kingesababisha mashabiki wengi wa kombe lijalo la dunia, kutokwenda Afrika Kusini ?

Afrika kusini,haikuwahi kutawaliwa vibaya tangu kujikomboa kwake miaka 16 iliopita kama hivi sasa.Ndio maana kwa kuuwawa Terre Blanche ,mtetezi wa siasa za ubaguzi na mtengano ,kiroja cha mambo, kunatoa fursa mpya kwa Afrika kusini mpya na ya rangi mbali mbali kupambana na wachochezi wanaoikaba roho hivi sasa nchi hii.Hii ikifanikiwa, kifo cha Terre Blanche,licha ya picha zote za maudhi kwenye TV,kitaleta kitu kidogo cha nafuui.

Mwandishi: Schadomsky,Ludger

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Uhariri: Sekione Kitojo