1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini: Mahakama yatoa uamuzi wa kesi dhidi ya Zuma

29 Desemba 2017

Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imesema bunge la nchi hiyo halikutimiza sharti la kumuwajibisha rais Jacob Zuma kuhusiana na kashfa ya matumizi ya fedha ya umma

https://p.dw.com/p/2q5rp
Südafrika Präsident Jacob Zuma
Picha: picture-alliance/dpa/N. Bothma

Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imesema bunge la nchi hiyo halikutimiza sharti la kumuwajibisha rais Jacob Zuma kuhusiana na kashfa ya matumizi ya fedha ya umma kukarabati nyumba yake binafsi.

Hukumu hiyo ndiyo pigo la karibuni zaidi la kisheria kwa rais Zuma, ambaye anakabiliwa na shinikizo kubwa la umma kumtaka aondoke madarakani katika taifa hilo la Afrika lililopiga hatua kiviwanda kabla ya uchaguzi mkuu wa 2019. Lakini haikubainika mara moja, ni hatua zipi bunge litachukuwa.

Chama cha wapigania uhuru wa kiuchumi EFF, pamoja na vyama vingine vidogo vya upinzani ndivyo viliyvopeleka suala hilo la kikatiba katika mahakama.

Zuma mwenye umri wa miaka 75, yuko katika nafasi dhaifu baada ya makamu wa rais Cyril Ramaphosa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha African National Congress ANC, ingawa bado kikundi chake kinashikilia nafasi muhimu katika chama, na amekuwa akiepuka mara kadhaa kura ya kutokuwa na imani naye.