1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yakosolewa juu ya msimamo wake kuhusu Libya

8 Septemba 2011

Kitendo cha Afrika ya Kusini kutolitambua Baraza la Mpito la Waasi la Libya kunadhihirisha urasimu wake mkubwa katika kutoa maamuzi. Urasimu huo unaweza kuharibu sifa na ushawishi wake barani Afrika.

https://p.dw.com/p/12UtR
Rais Jacob ZumaPicha: dapd

Afrika Kusini imelidharau baraza la waasi. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema haitekelezi vyema na kwa uhakika siasa zake za nje jambo ambalo linaweza kulipeleka kombo taifa hilo.

Gary van Staden, mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa taasisi ya masuala ya uchumi ya NKC Independent Ecomists anasema hali hiyo inalifanya taifa hilo lijeweke lenyewe katika muelekeo mbaya.

Anasema kama hawajachuka hatua kwa hivi sasa na kujihusisha mapema kuna uwezekano mkubwa wa taifa hilo kupoteza ushawishi wake katika nchi nyingi barani Afrika.

Muammar al Gaddafi / Libyen
Muammar GaddafiPicha: dapd

Afrika Kusini imekuwa ikimuunga mkono Muammar Gaddafi na imekuwa na uhusiano wa karibu na wa muda mrefu.

Wakati wa vuguvugu la ubaguzi wa rangi, Libya ilikuwa nchi pekee kukisaidia chama tawala cha Afrika Kusini ANC kupambana na kundi la weupe walio wachache nchini humo.

Safari ya kwanza ya Gaddafi, baada ya kuondolewa vikwazo ilikuwa ya Afrika ya Kusini wakati wa utawala wa Nelson Mandela na Mandela alikuwa akimwita Gaddafi kaka yake.

Zaidi ya mataifa 60 yamelitambua baraza la mpito la waasi na hivi karibuni China ilisema italitambua baraza hilo kuwa ni chombo halali cha kuwawakilisha wa wananchi wa Libya.

Serikali ya Afrika ya Kusini imeendelea kusisitiza kwamba matatizo ya Waafrika yanapaswa kutatuliwa na wenyewe kwa kupitia chombo chake, Umoja wa Afrika.

Na nchi hiyo kama kiungo muhimu katika umoja huo bado haijalitambua baraza la mpito la waasi. Umoja wa Afrika nao pia mpaka sasa haujalitambua baraza hilo.

Gaddafi anatazamwa kama mtu muhimu aliyeshiriki katika kuunda Umoja wa Afrika nzima, ikiwa moja kati ya mafanikio makubwa.

Nel Marais, Mkurugenzi Mkuu wa asasi ya ushauri wa kukabiliana na majanga amesema ukiritimba unaojitokeza katika serikali ya chama tawala cha ANC ni tatizo kubwa.

Anasema watunga sera wanapaswa kukusanya mawazo tofauti kutoka katika wizara mbalimbali na idara kabla ya kupitishwa maamuzi yoyote. Anasema hiyo inamaanisha serikali haiwezi kukurupuka katika mambo muhimu.

Marais anasema kunahitajika idara, kamati na watu binafsi ili kuweza kupata usahihi wa jambo kabla ya kubadilisha kitu chochote.

Wachambuzi wametoa mfano mwingine ambao Afrika Kusini inajiburuza katika kuufikisha tamati, ni kuendelea kumuunga mkono kiongozi wa muda mrefu nchini Zimbabwe Robert Mugabe.

Pamoja na hali hiyo pia wanailaumu kwa kuchelewa kumtambua rais Alassane Outtara wa Cote d'Ivoire baada ya uchaguzi uliosababisha machafuko nchini humo.

Mchambuzi mwingine Mike Dave alizungumzia kitendo cha nchi hiyo kuungana na Brazil, Urusi, India na China kutolipigia kura azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa lililokuwa na lengo la kuwalinda raia wa Libya na badala yake ikawa inalalamikia makombora ya anga ya jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Mwandishi: Sudi Mnette//RTR
Mhariri:Josephat Charo