1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika Kusini

Afrika Kusini yawasilisha hoja zake ICJ dhidi ya Israel

11 Januari 2024

Afrika Kusini leo imeituhumu Israel kufanya "mauaji ya halaiki" dhidi ya jamii ya Wapalestina na kuitaka mahakama ya kimaitafa ya mjini the Hague.

https://p.dw.com/p/4b8Aa
Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini Ronald Lamola na Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi Vusimuzi Madonsela kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)
Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini Ronald Lamola na Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi Vusimuzi Madonsela kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)Picha: REMKO DE WAAL/ANP/AFP/Getty Images

Katika siku ya kwanza kati ya mbili ya kusikilizwa kwa kesi iliyofunguliwa na Afrika Kusini kwenye mahakama ya Umoja wa Mataifa, ICJ, mawakili wa nchi hiyo wamesema mashambulizi ya anga na ya ardhini yanayofanywa na Israel huko Gaza yanalenga kuiangamiza jamii yote ya Wapalestina kwenye ukanda huo.

Israel imepuuza madai hayo ikiituhumu Afrika Kusini kufanya kazi ya kuwa "wakili" wa wanamgambo wa Hamas na kuitaja kesi ililoifunga kama moja ya "onesho la aina yake la tabia ya undumilakuwili".

Jopo la majaji 15 wa mahakama ya ICJ watatoa uamuzi kuhusu shauri hilo mwezi ujao lakini haitakuwa na nguvu yoyote ya kuutekeleza.