1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Afrika si hatari kuwekeza"

Admin.WagnerD24 Januari 2013

Kutokana na ukuaji wa viwango vya ustawi vinavyoshindana na Bara la Asia na kutokana na uwezo ambao bado hajuanza kutumika kabisa, Afrika sasa imeondokana na ile shaka ya kwamba ni mahala hatari kwa uwekezaji.

https://p.dw.com/p/17QhP
Jacob Zuma, Präsident Südafrika auf dem WEF 2013Quelle: WEF Frei zur Verwenung für Pressezwecke Aufnahme: 23.1.2013, Davos, Schweiz
Rais Jacob Zuma wa Afrika KusiniPicha: WEF

Kauli hiyo ya viongozi wa mataifa iliyotolewa katika kongamano la kimataifa la kibiashara linalofanyika Davos nchini Uswisi. Wakiwa wamekusanya katika mji wa mapunziko, Davos, viongozi wa Afrika wamesema pamoja na kwamba bado kumekuwa na mikingamo kadhaa likiwemo tatizo la miundombinu na tatizo la ajira kwa vijana lakini uhuru wa kuwekeza katika bara hilo sio tatizo tena.

Akizungumza na jopo la wataalamu wa kuangalia ustawi wa Afrika "De-risking Africa" rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alihoji kwamba " Ni kweli Afrika ni hatari kuliko eneo lolote duniani". Kiongozi huyo aliendelea kwa kusema mtazamo huo unapaswa kufanyiwa kazi.

Hatua imepigwa barani Afrika

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kuna ushahidi kwamba bara hilo linasonga mbele sambamba na uwepo wa ushahidi kwamba viongozi wa Afrika wanafanya jitihada za pamoja katika kufanya mambo yatakayolisaidia bara hilo kusonga mbele.

Naye Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria aliunga mkono maneno ya Jacob Zuma kwa kusema Afrika isitengwe katika biashara yeyote, uwekezaji na wowote na kusisisitiza hatari katika biashara haipo Afrika tu, bali kokote ulimwenguni inaweza kutokea.

1, Goodluck Ebele Jonathan, Präsident Nigerias auf dem WEF 2013 Quelle: WEF Frei zur Verwenung für Pressezwecke Aufnahme: 23.1.2013, Davos, Schweiz
Rais Goodluck Jonathan wa NigeriaPicha: WEF

Rais huyo wa Nigeria alisema kabla ya wakati huu, mataifa mengi ya Afrika hayakuwa na utulivu wa kisiasa lakini kwa sasa mataifa mengi yamekuwa madhubuti kwa hivyo biashara inaweza kufanyika.

Jitihada za kukuza uchumi zinahitajika

Kwa mujibu wa Shirika la Fedha Duniani IMF uchumi wa Afrika ungaliweza kukua kwa asilimia tano kwa mwaka uliyopita yaani 2012 na asilimia 5.7 kwa mwaka huu wa 2013. Katika utabari huo mataifa yalitajwa uchumi wake kuongezeka ni pamoja na Ghana, Cote d'Ivoire, Nigeria, Angola na Gabon.

Hata hivyo pamoja na eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kuchangia kiasi cha asilimia 2.5 katika pato la ndani ya dunia bado kuna safari ndefu katika ukuaji wa kiuchumi. Hakika kilio kikubwa bado kimebaki katika suala la miundo mbinu, ambapo viongozi wa wanaohudhuria mkutano huo wamelalamikia tatizo la barabara, hasa kuanzia ndani ya nchi zenyewe husika, tatizo la umeme na upatikanaji wa maji.

Rais Jonathan amedokeza kwamba sula la miundombinu ni muhimu wakati Rais Jacob Zuma alisema viongozi wa Afrika wanafanya kazi kwa pamoja katika kushughulikia miundombinu kwa kutoa mfano wa mradi Grand Inga Dam huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Viongozi hao pia wametaja juu ya jitihada za pamoja za kurejesha utulivu katika bara hilo na hasa wa kutolea mfano juhudi za Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) katika mzozo wa Mali. Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambae nchi yake inajivunia kasi ya ukuaji wa uchumi alisema uwajibikaji katika uongozi bara la Afrika unahitajika sana katika kutatua matatizo ya ndani ya bara hilo.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman