1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yaathirika zaidi na rushwa

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYsA

BERLIN

Utafiti wa Shirika la Kimataifa la kupiga vita rushwa duniani Transparency International lenye makao yake mjini Berlin Ujerumani limebaini kwamba watu maskini ndio wanaoathirika zaidi na rushwa duniani.

Orodha hiyo itolewayo kila mwaka ya kipimo cha rushwa duniani imeiorodhesha Afrika kuwa ndio bara lililoathirika zaidi ambapo asilimia 42 ya watu waliohojiwa wamesema kwamba wanatakiwa watowe hongo ili kuweza kupatiwa huduma za afya na elimu.

Huguette Labelle ni mwenyekiti wa Shirika la Transparency International.

Watu 63,000 wameshiriki kwenye uchunguzi wa maoni uliofanywa katika nchi 60 duniani.